The House of Favourite Newspapers

Tonombe, Tuisila Waipa Jeuri Yanga

0

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umejitapa kufanya vyema msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kufuatia kukamilisha usajili wa nyota kadhaa wa kigeni wakiwemo Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe wa AS Vita ya DR Congo.

 

Yanga imefanya usajili wa wachezaji tisa hadi sasa wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kufanya maboresho ya kikosi chao ili kuleta ushindani kwenye msimu wa 2020/21.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa usajili walioufanya safari hii si wa kitoto ambao haujafanywa katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo.

YANGA

“Yanga imejipanga kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu, tumefanya usajili makini ambao hatujafanya kwa misimu mitatu mfululizo hivyo tunaamini wachezaji tuliowasajili wataleta ushindani wa kutosha kwenye ligi.

 

“Wachezaji tuliowasajili wote wana viwango vizuri, hivyo tumekuja kwa lengo la kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa ligi msimu ujao kwa kuhakikisha tunafanya vyema katika kila mechi.

 

“Mechi ya siku ya kilele cha Wananchi itakuwa ni mwanzo mzuri kwetu kuelekea katika ligi kuu ili kuona tunapata mafanikio.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Leave A Reply