The House of Favourite Newspapers

Tonya: Tulitaka Tumzike Gigy Money

Matonya

Matonya.

WAFUATILIAJI wa burudani hususan katika Muziki wa Bongo Fleva watakuwa wanazifahamu nyimbo kama Vaileth, Anita, Taxi Bubu na Dunia Mapito ambazo zilifanya poa katika chati na sehemu mbalimbali za starehe. Mkali wa ngoma hizo alikuwa ni Seif Shaban maarufu kama Matonya. Jamaa huyu ni mmoja wa wanamuziki wakongwe wanaoendelea kulisongesha katika gemu la muziki wa Bongo Fleva ambapo anapoibuka na ngoma mpya huwa gumzo. Kama utakumbuka miaka miwili iliyopita alikuwa akitesa na Ngoma ya Mule Mule aliyomshirikisha Rich Mavoko, akafunga mwaka jana na Sugua Benchi na sasa amefungua mwaka na ngoma mpya ya Hakijaeleweka ambapo ndani ya ‘kideo’ chake yumo muuza nyago Gigy Money.

matonya

Gigy Money na Matonya

Juzikati Matonya alitimba ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na kupokelewa na Global TV Online kisha kufanyiwa mahojiano katika Kipindi cha Exclusive na katika makala haya anafunguka zaidi;

matonya-1

Matonya

 Showbiz: Hongera kwa kazi zako, lakini ujio wako safari hii upo kasi sana. Umefunga mwaka na Sugua Benchi na umefungua na Hakijaeleweka, kwa nini umetoa ngoma haraka hivi kwa kipindi kifupi?

 Matonya: Ujue maisha yanabadilika! Mashabiki wangu walikuwa wamemiss sana kumsikia Matonya kila mara akiwa na nyimbo tofauti. Hivyo mipango yangu ni kuwafurahisha kwa kutoa nyimbo nyingi na kwa haraka zaidi.

gigy_money

Gigy Money

Showbiz: Kuna utofauti gani kati ya Matonya wa zamani na sasa?

 Matonya: Matonya wa zamani na sasa ni watu wawili tofauti. Mfano ukiangalia video ya wimbo wangu huu mpya wa Hakijaeleweka ni tofauti na za nyuma. Nimeonesha maisha ya watu wengi wasivyothamini mtu wa pembeni hadi anapoondoka (kufariki) ndo’ wanajua thamani yake. Nimeonekana nipo makaburini nasali kwa uchungu kitu ambacho sijawahi kukifanya katika video zangu za nyuma.

 Showbiz: Unaweza kutuambia ilikukosti kiasi gani maandalizi ya hii video?

 Matonya: Nashukuru haikutukosti kiasi kikubwa video hii japo siwezi kukitaja kwa sasa lakini kuna vitu vidogovidogo kiukweli vilitukosti kama vile kuna sehemu za makaburini ilibidi tukodi kisha tusubirie hadi vibali yaani process ilikuwa ndefu sana.

 

matonya

Matonya

 Showbiz: Katika video yako kuna video queen Gigy Money ameonekana kubadilika kimavazi, sijui unaweza kutuambia ilikuwaje?

 Matonya: Kikubwa nilitaka kubadilisha mazingira ya Gigy kwa maana watu wengi wamezoea kumuona kwenye video na nje ya video akiwa katika mavazi ya nusu utupu. Nimejaribu kumbadilisha na kuonesha jamii kuwa ukiishi na wanawake kama hawa wanaweza kubadilika.

Najivunia sana kwani kwa upande wa video, Gigy ameweza kufunika kwa kiasi kikubwa kutokana na mavazi ya heshima aliyoyavaa mwanzo hadi mwisho yaani sasa hivi kwa walioiona video hii wakimuona Gigy alivyo wanaweza kuleta hata ng’ombe, mbuzi au hata wakajenga ghorofa kwa ajili ya kumchumbia.

Gigy-money-(5)

Gigy Money

Showbiz: Ugumu gani mliupata wakati mnatengeneza video?

Matonya: Dah! Ujue wakati tunatengeneza kwanza, tulitaka Gigy adumbukizwe (azikwe) katika kaburi lililochimbwa kwa mujibu wa ‘skripti’. Kabla ya kufanyika video, Gigy alinipigia simu na kuniuliza nguo zipi sasa anaweza kuzikiwa nazo lakini tukawa tumebadilisha idea hiyo na kuonesha tayari ameshazikwa na kaburi limetengenezwa.

 Showbiz: Kwa sasa nani anasimamia kazi zako za muziki?

 Matonya: Namshukuru Mungu nina mameneja watatu, wa kwanza Kapasta 4 Real, James na Hilton ambaye yupo Nairobi kwa ajili ya kunisimamia nje ya mipaka.

Gigy money (6)

Gigy Money na Mwanahabari.

Showbiz: Unazungumziaje janga la madawa ya kulevya lililowakumba wasanii wengi kwa sasa?

Matonya: Kiukweli hali inatisha na vijana wengi wanaangamia lakini wa kuwaokoa ni sisi wasanii pamoja na jamii. Ni lazima tushirikiane kwa pamoja kuweza kutatua janga hili. Kama tunaweza kushirikiana katika kuingia studio na kutoa nyimbo kali kisha kushirikiana na media basi hata hili la kuwaokoa vijana wenzetu tukishirikiana tunaweza kuliepuka.

 

Comments are closed.