The House of Favourite Newspapers

TRA Yataja Viwango Vipya Kodi ya Majengo Inayotozwa Kupitia Luku

0

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza viwango vipya vya kodi ya majengo vinavyokusanywa kwa kutumia njia ya ununuzi wa umeme kwa wamiliki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRA Mei 4, 2023 viwango vya utozaji kodi ya majengo kwa mujibu wa mabadiliko ya kifungu cha 6 Cha Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa (ukadiriaji), yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Na. 3 ya 2021.

Viwango hivyo vipya ni pamoja na, kiasi cha Sh. 12,000 kwa mwaka kwa nyumba ya kawaida. Sh. 60,000 kwa mwaka kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa katika maeneo ya majiji, manispaa na halmashauri.

Nyumba ya ghorofa katika maeneo ya halmashauri za wilaya, itatozwa kiasi cha Sh. 60,000 Kila mwaka.

Awali, kiwango cha kodi hiyo ilikuwa Sh. 12,000 kwa majengo yote.

Taarifa ya TRA imesema kuwa, kwa sasa uhakiki wa majengo ya ghorofa unaendelea kufanyika na Miata husika kuwekewa kiwango stahiki kulingana na aina ha jengo.

TRA inakusanya kodi hizo kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

ALLY KAMWE ANAONGEA NA WAANDISHI MUDA HUU, MIPANGO KUELEKEA MECHI DHIDI YA MALUMO GALANT…

Leave A Reply