The House of Favourite Newspapers

TRC Yaanika Usiyoyajua Kuhusu Ujenzi wa Reli ya Umeme – Video

Shirika la Reli  Tanzania (TRC) limeeleza mafanikio mbalimbali ya shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa kwa ajili ya treni za umeme pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 14, kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kwa upande wa wataalamu 189 ni Watanzania na 258 ni wageni.

 

Kadogosa amesema TRC inajenga madaraja makubwa maeneo mbalimbali nchini na kwamba wanajipanga kujenga reli ya kisasa kwa mikoa yote Tanzania lakini kutokana na vifaa kuwa na uzito mkubwa ambao unaweza kuathiri barabara, wamejipanga kutumia reli za zamani zilizopo.

 

Aidha, amesema zaidi ya watu 6,000 wameajiriwa katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR). Kati ya ajira hizo asilimia 96 sawa na watu 6,182 ni za Watanzania na asilimia nne sawa na watu 258 ni wageni.

 

“Ajira 626 za Watanzania wasio na ujuzi na 19 za wenye ujuzi zimepatikana kupitia kampuni za wazawa wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huu, hivyo tunafanya vizuri sana,” amesema Kadogosa.

 

Amesema maendeleo ya ujenzi huo kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro yamefikia asilimia 34. Kipande hicho chenye urefu wa kilomita 300 kilianza kujengwa Mei 2, mwaka jana na kinatarajiwa kukamilika Novemba 2, mwakani.

TAZAMA VIDEO HII HAPA

Comments are closed.