The House of Favourite Newspapers

Treni Yawaka Moto, 16 Wafariki Dunia

WATU 16 wamefariki baada ya treni ya mwendokasi kuwaka moto na wengine 13 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo huko Liaqatpur karibu na mji wa Rahim Yar Khan.

 

Waziri wa Masuala ya Usafirishaji wa reli, Sheikh Rashid Ahmad amesema moto umesababishwa na jiko la gesi lililopuka wakati abiria wakipika chai, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

 

Treni hiyo ilikuwa inatokea Lahore kwenda Karachi. Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya karibu huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

 

UPDATE: Kwa mujibu wa The Associated Press, Maafisa wa Uokoaji wa Pakistani wamesema idadi ya vifo vilivyotokea kwenye treni iliyowaka moto vimefikia 62 – Aidha, Watu wengi wamejeruhiwa na kati yao wengi wao wapo mahututi. Shughuli za uokoaji zinaendelea.

 

Comments are closed.