The House of Favourite Newspapers

Mataifa Sita ya Afrika Yaliyowahi Kubadilisha Majina! – Video

KAMA ulikuwa hujui bas daka hii! Zimbabwe ilijulikana kama Rhodesia kusini kati ya mwaka 1898-1964, ambalo ni jina la Mkoloni wa Uingereza Cecil Rhodes.

 

Mapema 1960, raia wenye utaifa walianza kuliita taifa hilo Zimbabwe. Jina linalotokan ana maneno mawili dzimba na dzamabwe yenye maana ya nyumba ya mawe kwa lugha ya Shona inayozungumzwa pakubwa hivi leo Zimbabwe.

 

Rais Thomas Sankara, kiongozi mshupavu na kijana awali ilijulikana kama Upper Volta, alilipa taifa hilo jina rasmi la Burkina Faso mnamo August 1984.

 

Alilichagua jina hilo ambayo ni maneno mawili Burkina na Faso kutoka makabila mawili makuu yanayozungumzwa nchini humo.  Jina la zamani la Upper Volta lilitoka kwa Ufaransa iliyokuwa mkoloni kutokana na mto wa Volta uliopita katika eneo hilo.

 

Burkina katika lugha ya Mòoré lina maana wanaume wenye heshima na Faso katika lugha ya Dioula lina maana alikozaliwa baba yakichanganywa, Burkina Faso lina maana eneo la watu wa kweli.

 

Comments are closed.