The House of Favourite Newspapers

Trump Awatimua Wasomali 90 na Wakenya 2 Marekani

trump14Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.
Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.
Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.
Nchi hizo ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen 

Comments are closed.