The House of Favourite Newspapers

Tshabalala Achimba Mkwara Mzito Simba

0

 

Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’

BEKI wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amefunguka kuwa kamwe hatakubali kuona anapokonywa nafasi yake kirahisi na mchezaji yeyote wa timu hiyo. Tshabalala ameyasema hayo kufuatia Simba kumsajili aliyekuwa beki wa Mbao FC ya Mwanza atakayeshindana naye, Jamal Mwambeleko, kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Tshabalala ambaye ametajwa kuwa mchezaji bora wa Simba msimu huu, alisema siku zote amekuwa akifuata utaratibu aliojiwekea katika mchezo wa mpira kwa kuwa amekuwa hapendi kuona akirudishwa nyuma na mtu atakayekuwa anataka kuchukua nafasi yake.

 

“Hii yote imetokana na suala zima la nidhamu na kujituma kwa sababu siku zote nimekuwa sipendi kuona nikivunja miiko yangu katika mchezo wa soka ambayo nimejiwekea, kwa sasa natakiwa niendelee kufanya zaidi ya nilipofikia ili nizidi kuwa bora.

 

“Unajua mimi ni mchezaji na sitakiwi kumuhofia mchezaji yeyote katika timu yetu, najua kuwa hivi sasa timu inafanya usajili kwa ajili ya msimu ujao, naamini ushindani wa namba utakuwa mkubwa ila niseme tu kwa upande wangu kama nitaendelea kuwa mzima basi sitakubali kupokonywa namba,” alisema Tshabalala ambaye pia ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Julio Awaka Akirejesha Fomu, Ataka Wanaojua Mpira Ndiyo Wapewe Uongozi TFF

Leave A Reply