The House of Favourite Newspapers

Tshisekedi Awasamehe Waliomuua Rais Kabila

0
Kanali Eddy Kapend alikanusha kuhusika na mauaji ya Rais Kabila.

 

 

WANAUME wawili waliopatikana na hatia ya mauaji ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent Kabila, miaka 20 iliyopita wamepewa msamaha.

 

Japo Kabila alipigwa risasi na mlinzi wake, maafisa wake wawili wa ngazi ya juu, Kanali Eddy Kapend na Georges Leta, walihusishwa na mauaji hayo. Rais FĂ©lix Tshisekedi alibadilisha hukumu ya kifo dhidi yao mwezi Juni mwaka uliyopita.

 

Hatua hiyo inajiri wakati kuna mvutano kati ya Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila ambaye ni mwana wa kiume wa Laurent Kabila.

 

Joseph Kabila alichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake mnamo 2001 na alitawala Congo kwa miaka 18 kabla ya Tshisekedi kushinda uchaguzi mnamo Desemba 2018.

 

Ingawa ulikuwa upokezanaji wa madaraka wa kwanza wa amani nchini humo kwa karibu miaka 60, wengi walipinga matokeo ya uchaguzi.

 

Kumekuwa na tuhuma kali kwamba rais huyo mpya alifanya makubaliano ya nyuma ya pazia na Joseph Kabila, ambaye bado ana ushawishi mkubwa nchini.

Ofisi ya Tshisekedi ilisema msamaha wa rais ulitolewa kwa kila mtu aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani na ambao walikuwa wametumikia vifungo vyao kufikia tarehe 31 Desemba.

 

Giscard Kusema, wa ofisi ya habari ya rais, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Kanali Kapend na watuhumiwa wenzake “wananufaika na msamaha wa urais …. ambayo ni kipimo cha upeo wa jumla na tabia isiyo ya kibinadamu”.

 

Kanali Kapend alikuwa mtumishi wa karibu wa Laurent Kabila. Alipatikana na hatia ya kupanga mauaji, pamoja na maafisa wengine kadhaa wa kitengo cha usalama cha marehemu rais, pamoja na mkuu wa upelelezi wa wakati huo Georges Leta. Wote wawili walipinga kuhusika na njama hiyo.

 

Msamaha huo wa rais umetolewa wiki chache baada ya Tshisekedi kuvunja muungano wake na chama cha Kabila – kilicho na wabunge wengi – baada ya kuongezeka kwa taharuki. Rais kwa sasa anatafuta washirika wapya watakaoungana naye ili apate kuwa na wabunge wengi ndani ya bunge.

Leave A Reply