Tsunami Yaua Watu zaidi ya 160, Zaidi ya 700 Wajeruhiwa

TAKRIBAN watu 168 wameuawa na wengine 745 kujeruhiwa baada uya tsunami kuikumba miji ya pwani nchini Indonesia kwa mujibu wa serikali nchini humo.

Mawimbi ya tsusami yaliwasili usiku bila onyo lolote, na kuharibu mamia ya nyumba.

Maofisa wanasema tsunami hiyo huenda ilisababishwa na maporomoko ya ardhi chini ya bahari baada ya kulipuka kwa volkano ya Anak Krakatau.

Eneo la Sunda Strait kati ya visiwa vya Java na Sumtara huunganisha bahari ya Java na bahari ya Hindi.

 

Idara inayohusika na majanga imeonya watu kukaa mbali na pwani kutokana na hofu kuwa tsunami nyingine inaweza kutokea.

Tsunami ya Jumamosi ilipiga fukwe kadhaa likiwemo eneo la kustarehe la Tanjung Lusung magharibi mwa kisiwa cha Java.

Vifo vimeripotiwa maeneo ya Pandeglang na Serang huko Java, na mkoa wa Lampung huko Sumatra. Maofisa wanahofu kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.

Loading...

Toa comment