The House of Favourite Newspapers

TTCL Yadhamini Bonanza Soka la Vyuo Ufukweni

1Kocha mkuu wa timu ya taifa kwa soka la ufukweni, John Mwansasu,  akizungumza na wanahabari.

2Mratibu wa bonanza hilo, Dimo Debwe (kushoto) akizungumza kwenye hafla hiyo.

3Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota, akifafanua jambo.

4Baadhi ya wandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

KAMPUNI ya mawasiliano nchini (TTCL) imedhamini bonanza la mchezo wa soka la ufukweni kwa timu za vyuo vya jijini Dar es Salaam lenye lengo la kuunda timu imara ya taifa kwa mchezo huo.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Peter Ngota, alisema lengo la kudhamini bonanza hilo ni kutambua kuwa michezo hujenga amani na furaha.
“TTCL inalenga hasa kuibua vipaji vya vijana wetu ili waweze kufikia malengo yao ya kisoka na kuja kuwa wachezaji wazuri watakaokuja kuisaidia timu ya taifa kwa mchezo huu,” alisema.
Naye kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania kwa soka la ufukweni, John Mwansasu, alisema katika bonanza hilo kutakuwa na timu zitakazokuwa na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga ili kuzipa nguvu na hamasa kwa mashabiki.
Alisema bonanza hilo linatarajiwa kufanyika Januari 7, mwaka huu katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Naye Mratibu wa bonanza hilo, Dimo Debwe, alivitaja baadhi ya vyuo vitakavyoshiriki bonanza hilo kuwa ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara (CBE), Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ), Chuo cha Usafirishaji (NIT), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Chuo cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.  Pia Debwe amewaomba wapenzi wa soka hilo kujitokeza kwa wingi kushuhudia bonanza hilo.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.