The House of Favourite Newspapers

Tumieni Mifumo ya Tehama Kuzuia Upotevu wa Mapato- Ndugulile

0

MBUNGE wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya cha Kigamboni kutumia mifumo wa Tehama katika kuhakikisha kuna udhibiti mzuri wa mapato yanayotokana na huduma zotolewazo katika kituo hicho.

 

Ndugulile ameyasema hayo Septemba 24, 2021 alipofanya ziara ya ukaguzi wa utoaji huduma katika kituo hicho ambacho alisomewa Taarifa ya mapato yanayokusanywa ndani ya kituo hicho ni Tsh Milioni 30 kwa mwezi.

 

“Natumbua kituo hiki ni cha pili baada ya hospitali ya Vijibweni kwa kuhudumia wagonjwa Wilayani Kigamboni. Hapa kuna huduma za X-Ray, Upasuaji, Ultra Sound na maabara, Sasa mnaponiambia kuwa kwa mwezi mnaingiza Tsh Milioni 30 pekee maana yake kwa siku ni Tsh Milioni 1. Hesabu hizi haziko sawa.

 

Niwakumbushe makubaliano yetu ya kufunga mifumo ya TEHAMA kwenye vituo vya kutolea za afya Kigamboni. Mifumo hii itasaidia sana kudhibiti upotevu wa mapato na kuboresha huduma za afya”. Alisema Ndugulile.

 

Aidha, amewataka wauguzi wa kituo hicho kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa kwani suala la lugha chafu ni moja ya kero aliyoelezwa na wananchi wa Kigamboni.

 

“Napenda kuwakumbusha watumishi wa afya kutumia lugha zenye staha kwa wagonjwa, kwani lugha ya staha ni sehemu ya maadili katika sekta ya afya, Leo nimekuja kuwakumbusha na nisingependa kusikia kero hii inaendelea” Alisema Ndugulile.

Leave A Reply