The House of Favourite Newspapers

Mechi Ya Simba Vs Yanga, Gazeti la Championi Lagombaniwa

0
Shabiki wa Timu ya Yanga akisoma Championi Kabla ya kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya Simba Vs Yanga.
Msomaji wa Gazeti la Championi akiuziwa gazeti hilo na Ofisa Masoko wa Global, Mwanahamis Khalid (kushoto).
Shabiki wa Timu ya Yanga akifurahia baada ya kukutana na Ofisa Masoko wa Global, Mwanahamis Khalid.
Timu ya Maofisa Masoko wa Global, kutoka kushoto ni Jimmy Haroub, Mwanahamis Khalid na Juma Johanes wakiwa katika Viunga Vya Uwanja wa Mkapa.

Mashabiki wa Timu ya Yanga wakipitia kusoma Gazeti la Championi kabla ya kuingia katika mtanange wa Simba Vs Yanga.
Muuzaji wa Magazeti ya Kampuni ya Global Publishers (kulia) akizunguka katika maeneo ya Uwanja wa  Mkapa Jijini Dar es Salaam kukutana na kuuza magazeti ya Championi.
Wakati Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania wakimiminika katika uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya watani wa jadi Simba na yanga wakipambana katika mchezo wa ngao ya Jamii, Timu ya masoko ya Global Publishers kupitia Gazeti lake pendwa la michezo la Champion imefika mapema katika Uwanja wa Mkapa kukutana na wasomaji wake  pamoja na kunadi gazeti hilo .
Mkuu wa kitengo Cha Masoko Global Publishers, Juma Johanes amesema lengo kubwa ni kukutana na wasomaji wa magazeti yetu ili kutengeza ukaribu zaidi na kuhakikisha magazeti yanawafikia kila mahali popote nchini.
“Sisi Kama Kampuni ya Global Publishers tunawahakikishia wasomaji wetu wa magazeti yote ya michezo, Championi na SpotiXtra kuwa tupo imara na tutaendelea kuwapa uhondo wa habari zote za michezo kwa wakati  kutoka ndani na Duniani kote”alisema Juma Johanes.
Leave A Reply