The House of Favourite Newspapers

‘TUNAFUNGA JUMLA-JUMLA 2018’: ROSTAM, MAUA SAMA WAAHIDI SAPRAIZ DAR LIVE

Wasanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki (kushoto)  Stamina (kulia)  na mwanadada, Maua Sama wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo juu ya shoo yao ya ‘Kufunga Mwaka Jumla-Jumla’ Dar Live  katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar.
Roma akizungumzia shoo hiyo na kuahidi sapraiz kibao.
Stamina  akiahidi kutowaangusha mashabiki watakaoingia ndani ya Dar Live usiku wa Mwaka Mpya Desemba 31 wiki ijayo.
Maua Sama ambaye anatamba na ngoma ya ‘Iokote’ akiahidi kuangusha bonge la shoo ndani ya kiwanja hicho.
Wanahabari wakiendelea kufanya yao.
Wasanii hao wakiwa na Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta almaarufu KP Mjomba (kushoto) na DJ Choka (kulia) ambaye anatarajiwa kuwa upande wa mitambo siku hiyo.

 

WASANII  wanaounda kundi la Rostam, ambao ni  Roma Mkatoliki,  Stamina na Maua Sama, leo wamewathibitishia wapenzi wa burudani kufanya shoo ya nguvu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar usiku wa kuamkia mwaka mpya 2019.

 

Nyota hao ambao watapiga shoo ya pamoja, wamesema katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar kwamba kama kawaida yao katika onyesho hilo hawataangusha mashabiki wa burudani na kuahidi sapraiz kibao za wasanii.

HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.