The House of Favourite Newspapers

Tunda; Hata Mume wa Mtu Naye ni Sumu

Anna Patrick Ki­mario, ‘ Tunda’

Anna Patrick Ki­mario wengi hawali­jui jina hilo na mara nyingi huwa najiuliza sijui kwa nini huwa hapendi uhalisia wa jina lake na kutaka ajulikane kwa jina la Tunda Sebastian.

Kuna wanaomjua zaidi na kusema kuwa amekulia mkoani Morogoro ingawa kuna wakati pia aliishi Moshi na Mtoni-Kijichi hapa Dar es Salaam, hiyo ilikuwa ni kabla hajaanza maisha yake ya kimjinimjini, maisha ya kiu­supastaa ambayo anaishi nayo sasa.

 

Tunda anajinasibu kwamba kazi inayomuweka mjini ni ‘U-video Queen’. Kwa wasioelewa maana yake, hawa ni wale wa­sichana wanaoonekana kwenye video za wasanii, hasa hawa wa Bongo Fleva.

Ukizungumzia kazi yake, japokuwa wengi wanaweza kuwa hawajui, lakini Tunda amefanya kazi kadhaa, japo siyo kivile lakini huwezi kumuondoa kwenye orodha ya wasichana ambao ukiwaweka kwenye video yako kama wewe ni msanii, basi hawezi kukuangusha.

 

Kazi yake mpya kabisa, ni kwenye video ya Barnaba aliyo­mshirikisha Aslay, iitwayo Ngo­ma. Zipo nyingine za kitambo kidogo ambazo Tunda amefanya kazi nzuri! Mnyonge mnyon­geni haki yake mpeni! Tazama video kama Why Me ya Amini na Barnaba, video ya wimbo wa Ma­tonya aliyomshirikisha Christian Bella uitwao Agwelina, mtazame kwenye video ya Raha ya TID!

Ninachotaka kukuonesha hapa ni kwamba japokuwa wengi hawamuelewi msichana huyu kama anajishughulisha na nini hasa, anacho kipaji, anayo kazi ambayo inamuingizia kipato na kama akiamua kuwekeza nguvu huko, anaweza kuishi mai­sha ya juu pengine kuliko haya anayofosi sasa.

 

U-video Queen au wengine wanaita Video Vixen, ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na upo ushahidi mkubwa wa watu waliofanikiwa sana kwa kazi hiyo, mfano mzuri ni kama mwa­nadada Tokyo anayeonekana kwenye video ya Kendrick Lamar iitwayo Backstreet Freestyle, au mwanadada mwingine Alisha Je­nay ambaye ameng’ara kwenye video kibao mbele, hasa za Hip Hop na kubwa kuliko ni mwana­dada Esther Baxter, kama humjui itazame video ya The New Work­out Plan ya Kanye West.

Baxter anatajwa kuwa ndiye Video Vixen mwenye mafanikio zaidi kwenye tasnia hiyo, hatua ambayo hata Tunda leo akiamua, anaweza kuifikia.

 

Unaweza kujiuliza, kwa nini namzungumzia Tunda? Huyu ‘mtoto’, licha ya umri wake mdo­go usiozidi miaka 24, ameshehe­ni matukio, tena mazitomazito!

Fuatilia akaunti yake ya Insta­gram, utagundua kwamba Tunda anapenda sana maisha ya juu, kutwa kucha kuzurura kwenye mahoteli makubwa, kazi yake kubwa ni kula bata! Tena kwenye viwanja vyenye hadhi ya juu!

 

Unaweza kujiuliza, ni pesa mbuzi anazolipwa na hawa wasanii wanaomtumia kwenye video zao ndizo zinazompa jeuri ya kutamba kiasi hiki? La hasha! Yapo madai mazito kwamba mwa­nadada huyu ameamua kutafuta mafanikio kwa njia ya mkato, anautumia mwili wake kama kitega uchumi!

Orodha ya wanaume wanaotajwa kubanjuka naye ni ndefu! Yupo Dia­mond Platnumz na wengine wengi, wakubwa kwa wadogo, mastaa kwa wasio mastaa!

Ninachotaka kukiweka sawa ni hili suala lililoibuka la kutoka kimapenzi na mtangazaji wa kituo kikubwa cha TV, Casto Dickson huku wakipa picha za kimahaba na kuziachia mitandao­ni.

 

Nilivyoona kwa mara ya kwanza nilishtuka kido­go nikaona huenda ni sehemu ya kutafuta kiki, mara ya kwanza niliona picha wakiwa katika Ukumbi wa Next Door kama sikosei ilikuwa ni kibao kata, ikaenea mtandaoni hata siku mbili hazikuisha nikaona tena picha wakiwa chumbani kwenye kioo tena wakiwa kwenye mapozi ya kima­haba, nikashtuka zaidi!  

 

Picha ziliendelea kumiminika hadi hivi ninavyokua­mbia, mbaya zaidi juzikati alifanyiwa mahojiano na moja ya gazeti hili na kukiri kuwa yupo katika uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo, akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yupo tayari kumzalia.

Wakati hayo yakiendelea limeibuka jipya la mzazi mwenziye na mtangazaji huyo aitwaye Don Posh ambaye pia ni Miss Aru­sha 2015 akiomba Tunda amuachie mzazi mwenzake kwa sababu bado yupo naye kwenye uhusiano na ame­shamzalia watoto mapacha.

 

Ninachotaka kukisema hapa, Tunda akiwa kama staa, kioo cha jamii ni vyema akajitathimini mwenendo wake, sitaki kuingilia sana huko lakini atambue uchungu wa mzazi huwa unauma sana, kutembea na mwanaume ambaye unajua kabisa ana uhusiano na mwanamke mwingine si jambo zuri. Watch out!

Comments are closed.