The House of Favourite Newspapers

IMEBAINIKA, KUMBE UNDANI WA UA JEKUNDU LA WEMA NI HUU!

MIONGONI mwa matukio yaliyotrendi kwa wiki hii ni hili la staa wa filamu Bongo mwenye hadhi ya nyota tano, Wema Isaac Sepetu ambapo alizua kizaazaa katika mitandao ya kijamii hususan Instagram baada ya kuposti picha ya ua jekundu kwenye ukurasa wake huku akisisitizia ishara ya upendo.

Kufuatia tukio hilo, mashabiki na watu wengi walielekeza hisia zao moja kwa moja kwa staa wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakiamini watakuwa wamerudiana baada ya staa huyo kuachana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

UA LILIPOANZIA

Kipindi ambacho kulianza kusikika taarifa za kurejea kwa mapenzi kati ya Diamond na Wema, ilikuwa kwenye utambulisho wa mwanamuziki Mbosso kwenye Lebo ya WCB uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro jijini Dar ambapo kulisambaa picha za wawili hao wakiwa kwenye pozi za kimahaba, zilizomkasirisha Zari na kuamua kuachia ngazi.

Zari, baada ya kuinua mikono juu aliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, ua jeusi na kuweka wazi kuwa uhusiano wake na mzazi mwenzake huyo umefikia mwisho na watabaki kuwa wazazi wa watoto wao wawili, Tiffa na Nillan na siyo mapenzi tena.

 

 

Kutokana na Zari kuweka ua jeusi kuashiria giza kwenye mapenzi, Wema naye akaweka ua jekundu kuonesha wazi ndiyo kwanza mapenzi yameanza kuchanua kwa upande wake.

MASHABIKI WAANZA KUJIWEKEA MAUA YAO

Baada ya Wena kuweka ua jekundu, iligeuka gumzo kubwa mitandaoni huku mashabiki mbalimbali kila mmoja akijiwekea ua lake, mwingine la kijani, mwingine bluu.

 

WEMA ANASEMAJE?

Gazeti hili lilimsaka Wema mara baada ya kuweka ua hilo kujua hasa sababu ya kuliweka na kuweka ishara ya upendo kulimaanisha amerudiana rasmi na Diamond au la ambapo simu yake iliita tu bila kupokelewa. Alipotumiwa ujumbe mfupi napo ulionesha kufika, lakini haukujibiwa.

 

MSEMAJI WAKE

Ijumaa halikulaza habari, lilimtafuta meneja ambaye pia ni msemaji wa Wema ambaye alipoulizwa kama anafahamu sababu za Wema kutumia ua hilo alisema:

“Ua aliloweka Wema kila mtu amelitafsiri tofauti, lakini aliamua kujiwekea tu picha yake anayoipenda na hakuwa na maana yoyote ya kuashiria yupo na nani kwa kipindi hiki.

Comments are closed.