The House of Favourite Newspapers

Tunda, Meja Wawajibu Wema, Whozu Waoneshana Mahaba ya Kufa Mtu

0
Video vixen maarufu Bongo, tunda akiwa na mpenzi wake msanii wa Singeli, Meja Kunta.

 

Tunda; ni video vixen maarufu Bongo na mzazi mwenza wa msanii Whozu ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na msanii wa Singeli, Meja Kunta.

 

Wakati huohuo, mpenzi wa zamani wa Tunda ambaye ni Whozu anatika kimapenzi na supastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu.

 

Sasa; Wema na Whozu wamekuwa wakioneshana mahaba ya kufa mtu huku wakiwataka wenye wivu wajinyonge, jambo ambalo limewaibua Tunda na Meja Kunta ambao nao wamejibu mapigo kwa mahaba tele na vijembe kama vyote.

 

Kinachofanywa na Tunda na Meja Kunta ni kuonesha kwamba nao mahaba yao si haba ili kutuliza upepo wa penzi la Wema na Whozu.

 

Wema na Whozu.

Imeelezwa kwamba, baada ya kuona mbwembwe za Whozu na Wema, nao Tunda na Whozu wameamua kukomesha kwa kujiachia watakavyo.

 

Zipo tetesi kwamba, katika sarakasi hizo zinazoendelea, Tunda na Whozu ndiyo wanateseka kwa sababu bado kila mmoja alikuwa anampenda mwenzake na ukitaka kutambua hilo, fuatilia mahojiano yao ambapo kila mmoja anaonekana kupaniki anapoulizwa kuhusu mwenzake.

 

Maswali wanayojiuliza wengi ni kwamba, yupo wapi mtoto wa Tunda na Whozu aitwaye Lolla kwa sababu mama yake yupo bize na Meja Kunta wakati baba yake yupo bize na Wema.

 

Kuhusu kumchukua baby mama wa rafiki yake ambaye ni Whozu, kwa upande wake Meja Kunta anasema; “Hata mimi marafiki zangu wamenichukulia wanawake zangu.”

UMAFIA YANGA YAMTEKA BOSS WA AL HILAL BONGO, SIMBA KUWAFUATA WA WAAONGOLA KITEMI | KROSI…

Leave A Reply