The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Akamatwa na Polisi, Aachiwa

0

ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi jioni ya bleo Jumatatu, Novemba 2, 2020 jijini Dar es Salaam.

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Lissu kwa madai ya kupanga maandamano.

 

Tundu Lissu amesema amekamatwa akiwa Umoja House jioni ya leo na sasa anafanyiwa mahojiano katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

 

Updates:

Aliyekuwa Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuputia Chadema, Tundu Lissu ambaye alikamatwa na jeshi la Polisi majira ya saa 12 jioni Umoja House, ameachiwa bila masharti baada ya mahojiano na Polisi. Ameachiwa yeye na aliokuwaameambatana nao.

Leave A Reply