The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu na Godbless Lema Watangaza Kurejea Nchini Muda Wowote Kufanya Kazi ya Siasa

0
Tundu Lissu

 

Makada wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Godbless Lema wamesema wanarudi nchini Tanzania muda wowote kuanzia sasa na kwamba hawarudi kukaa tu bali kufanya kazi ya Siasa.

 

Viongozi hao wa CHADEMA wamesema hayo wakati wakizungumza kwa njia ya mtandao na wanachama wa chama hicho mkoani Tanga

 

Makada hao ambao pia ni viongozi wa ngazi za juu kabisa kwenye chama hicho wamesema hayo wakati wakizungumza na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho kwenye Kongamano la 3 la vuguvugu la kudai Katiba mpya lililofanyika Jijini Tanga

Godbless Lema

 

Awali akizungumza moja kwa moja kwa njia ya mtandao kutoka nchini Ubeljiji, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba iwapo patafanyika masuala ya kiufunguzi na kiusalama basi atarejea nchini.

 

” Tunarudi wakati wowote kuanzia sasa, mimi tayari nimeshagawa hadi nguo za baridi japo huku Canada kwasasa hivi Baridi imepungua sana, jana (juzi) tulikuwa tunapanga na mwenzangu ni lini tuanze safari yakurudi nyumbani kwahiyo makamanda msiwe na wasiwasi tunakuja kuongeza nguvu za mapambano ya Katiba Mpya na Demokrasia kwa ujumla” Alisisitiza Lema

 

Kwenye kongamano hilo wanachama wa chama hicho na wananchi walipata fursa yakuuliza maswali ya moja kwa moja viongozi hao huku lengo kubwa la kongamano lilikuwa nikuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

 

Makamu Mwenyekiti huyo wa Chama hicho Tundu Lissu amesema katiba ya sasa haina nguvu na imetoa mamlaka makubwa kwa watawala waliopo madarakani na haina uwezo wakumuadhibu kiongozi wa ngazi za juu akiwa madarakani au baada ya kuondoka madarakani

 

Lissu amesema kwamba CHADEMA ndicho chama kitakachorudisha rasimu ya katiba ya jaji Warioba hivyo majadiliano yanaendelea na serikali imeonyesha nia ya kukubali kuanza mchakato wa Katiba mpya.

 

“Katiba ya Sasa hivi imefanyiwa marekebisho Mara 5, ukiangalia hata upatikanaji wake ulikuwa nitofauti kabisa na nchi nyingine kama Kenya, Katiba yetu ilipatikana ndani ya siku moja wakati wenzetu Kenya Katiba yao ilipatikana kwa miaka 3, ukiangalia tofauti hizi utagundua kuwa hii ni Katiba ya mkoloni sio ya Watanzania kwakuwa hawakuitolea maoni yao kama ilivyo Rasimu ya Warioba ” Amesisitiza Lissu

JUMA LOKOLE Afichua MAZITO, KAJALA Kwenda ZANZIBAR na HARMONIZE, PENZI la ESMA na COY, NDOA ya ZUCHU

Leave A Reply