The House of Favourite Newspapers

TUSUA MAISHA… NANI KUIBUKA MSHINDI DROO YA MWISHO?

PENALTI ya mwisho! Hebu vuta picha, wewe ni mchezaji wa mpira wa miguu, mpaka dakika tisini zinaisha hakuna mshindi, unawadia wakati wa penalti, wote wanapiga na inabakia moja ya mwisho ambayo ndiyo inayoenda kutoa matokeo ya mwisho! Utakuwa na hali gani kabla ya kupiga? Ukipiga halafu ukapata na kuipa timu yako ushindi utafurahi kiasi gani?

 

Basi hivyo ndivyo ilivyo kwenye shindano la Tusua Maisha na Global ambapo droo ya mwisho kabisa inatarajiwa kuchezeshwa Jumanne Septemba 11 na kuamua pikipiki ya mwisho inakwenda kwa msomaji gani. Hebu jiulize, kama utakuwa ni wewe utajisikiaje? Bila shaka shangwe zake hazielezeki.

 

Kizuri ni kwamba kila msomaji anayo nafasi sawa ya kuibuka mshindi! Huenda wewe unayesoma hapa ndiyo mshindi wetu wa mwisho! Changamkia magazeti ya Global, ujaze kuponi yako na kufuata maelekezo, huenda Jumanne yako ikawa poa sana baada ya kujishindia pikipiki mpya!

Wakati shindano likielekea ukingoni, jana washindi wa droo ya tisa na kumi walitarajiwa kukabidhiwa zawadi zao. Washindi hao ni Ramadhan Simba, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejishindia pikipiki, Anna Mbise wa Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliyejishindia jezi.

 

Wengine ni Ramadhan Mohamed wa Zanzibar aliyejishindia pikipiki, Geofrey John mkazi wa Chanika aliyejishindia dinner set na Justice Rugambwa mkazi wa Gongolamboto aliyejishindia zawadi ya jezi.

Lakini pia washindi wa droo ya kumi na moja ambao ni Bolen Kilimba aliyejishindia pikipiki, Silvanus Nyombe wa Mwanza aliyejishindia dinner set na Eliuter Ndunguru wa Manyoni, Singida, wao watakabidhiwa zawadi zao sambamba na washindi wa droo ya mwisho hivyo kuhitimisha safari ya kujishindia zawadi kedekede iliyodumu kwa muda wa wiki 12.

 

Ili kushiriki kwenye ‘penalti ya mwisho’, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra.

Ukishanunua, funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi.

Comments are closed.