The House of Favourite Newspapers

 Tx Junior ashindwa kumfikia Tx Moshi!

0

STAA wa Dansi anayeitumikia Msondo Music Band, Hassan Moshi ‘TX Junior’ amekiri kushindwa kufikia levo za kimuziki za baba’ke, marehemu Moshi William ‘TX Moshi’ ambaye naye aliitumikia bendi hiyo.

Katika exclusive interview na OVER ZE WEEKEND, TX Junior amefunguka kuwa, baba’ke pamoja na uimbaji, lakini pia alikuwa mtunzi mahiri, jambo ambalo yeye haliwezi.

“Nimeambulia kurithi kipaji chake cha kuimba tu, lakini nilichosh

indwa kurithi ni kipaji chake cha utunzi,” anasema TX Junior.

TX Junior amerithi kazi ya baba’ke kwenye bendi hiyo baada ya kufariki dunia, Machi 29, 2006 ambapo amekuwa akiwakosha anapoimba nyimbo za baba yake huyo ambaye wanafanana sauti.

 

STORI: RICHARD BUKOS

Leave A Reply