The House of Favourite Newspapers

U.T.I janga lisilopewa kipaumbele

0

Imekuwa ni kawaida kuambiwa fulani anaumwa U.T.I na watu wanachukulia ni suala la kawaida kutokana na kuwakumba watu wengi na ikumbukwe kuwa ugonjwa huu hushambulia zaidi akina mama kuliko wanaume.

Leo tutaanza kuangalia tatizo hili la U.T.I.

Tatizo la maambukuzi ya njia ya mkojo (Urinary Tract Infections) au kwa kifupi U.T.I kama ilivyozoeleka kwa wengi, kwa kiasi kikubwa, labda na hata wewe msomaji pengine ni zaidi ya mara moja umewahi kusikia mtu mzima au mtoto akiambiwa anasumbuliwa na U.T.I.

Kwa mtoto, mara nyingi si tabu sana na hakuna maswali mengi lakini kwa mtu mzima, kidogo mhusika mwenyewe, yaani mgonjwa na watu wa karibu naye wanakuwa na maswali mengi kuliko majibu.

U.T.I ni nini?

Maambukizi katika sehemu yoyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia U.T.I, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) ambao huishi katika utumbo mpana na kwa kawaida kama bakteria hawa huishi katika utumbo mpana basi kinyesi kinapotolewa nje kupitia njia ya haja kubwa bakteria hawa huwepo katika kinyesi na wengine hubaki katika ngozi hivyo kama mhusika atajisafisha kutoka nyuma kuja mbele ni rahisi bakteria hawa kuhamia katika njia ya mkojo na kushambulia mfumo huo hivyo maradhi haya hayata epukika.

U.T.I huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibaiolojia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo, huathiriwa zaidi na tatizo hilo.

Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa U.T.I na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili.

Vilevile kinga yao ya mwili bado huwa inakuwa haijakomaa kuweza kuhimili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na U.T.I hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bakteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani Urethra wa mwanamke ni mfupi sana ukiliganisha na wa mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.

Ukubwa wa tatizo

U.T.I ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo, hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneo mengi duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linalochongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la U.T.I huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata U.T.I japo mara moja. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya. N           ikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume. Unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply