The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Watishia Kuanzishwa Nchi Nyingine

0

CAMEROON inatarajia kufanya uchaguzi Desemba 6, mwaka huu licha ya kuwepo tishio la mapigano kutoka kwa makundi yanayotaka kujitenga na kuunda nchi yao.

 

Kundi linalotaka kujitenga ni la wanaozungumza Kiingereza ambao wanataka kujitofautisha na wanaozungumza Kifaransa. Kundi hilo limeanza mashambulizi dhidi ya maafisa uchaguzi.

 

Vikundi hivyo vimekuwa vikitahadharisha wagombea na jumuiya za kimataifa kuwa uchaguzi huo hautafanyika. Hivi karibuni, video imesambazwa mtandaoni ikionyesha mwanamme akitishia kuwaua wagombea wanaofanya kampeni.

 

Serikali imesema uchaguzi utahakikisha maslahi ya watu wanaozungumza Kiingereza yanatekelezwa kama ilivyokubaliwa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyoitishwa na Rais Paul Biya kati ya Septemba 30 na Oktoba 4, 2019.

Leave A Reply