UCHEBE: MKE WANGU ANANIONGEZEA UMRI

MUME wa msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Ashirafu Uchebe, amefunguka kuwa mkewe huyo anamwongezea siku za kuishi kwa sababu kila wakati humfurahisha. 

Akipiga stori na polisi wa Risasi Jumamosi, Uchebe alisema anashukuru Mungu amepata mke mwema ambaye anamfanya ajihisi mwanaume kamili na mwenye furaha muda wote.

“Mimi sitaki kuficha jamani, kwenye sifa lazima tuseme lakini mke wangu ni wa tofauti sana. Ananifanya najiona mwenye bahati, yaani mpaka nafikia mahali nafikiria ni wapi nilichelewa kumuona, maana mpaka sasa ningekuwa mbali sana kimaisha,” alisema Uchebe.

STORI: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment