The House of Favourite Newspapers

Ugonjwa Wa Kumuuwa Kajala Waanikwa

Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja.

Kila nafsi itaonja mauti na hakuna anayejua atakufa kifo cha staili gani, watu wa imani zote wanaamini hivyo lakini kwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja inadaiwa kwamba kama hatafuata masharti aliyopewa na daktari wake, kuna uwezekano mkubwa kifo chake kikasababishwa na matatizo ya moyo yanayomkabili. 

Chanzo makini ambacho kipo karibu kabisa na staa huyo, kilisema kuwa Kajala anasumbuliwa na tatizo la kusinyaa kwa moja ya valvu za moyo wake, ugonjwa ambao kitaalamu huitwa ‘Heart Valve Disease’ ambao alikuwa nao tangu zamani lakini alikuwa hajaligundua mpaka hivi k a r i b u n i alipozidiwa na kwenda h o s p i t a l i n i ambako ndiko alikoambiwa kuhusu ugonjwa huo.

kajala-1 Kajala akiwa katika pozi.

M p a s h a j i huyo aliendelea k u f u n g u k a kuwa baada ya kugundulika kuwa ana tatizo hilo, alitakiwa kuanza matibabu haraka huku akipewa masharti ya kuzingatia tiba na kubadili mfumo wa maisha yake, vinginevyo kifo kinaweza kumkumba.

 “Yaani kuna kipindi Kajala alikuwa hapati usingizi mpaka asubuhi huku akiwa na maumivu makali sana lakini watu walimshauri kuwa ni lazima aende hospitali kupimwa na alipoenda ndipo alipogundulika kuwa na tatizo hilo kwenye moyo wake,” kilisema chanzo chetu.

 Chanzo hicho kiliendelea kufunguka zaidi kuwa, pamoja na kupewa dawa lakini alishauriwa sana kufanya mazoezi ili kuupa moyo wake nguvu zaidi na asiache kufanya hivyo kwa kuwa kutamletea athari kubwa, ikiwemo kupoteza maisha ghafla. 

“Kajala sasa hivi mazoezi kila siku ndiyo tiba yake sahihi na hatakiwi kuacha kufanya hivyo kwa sababu ndiyo kitu kinamfanya kuwepo vizuri mpaka hivi sasa,” alisema rafiki huyo. Chanzo kiliendelea kueleza kuwa pamoja na mazoezi na dawa anazotumia lakini staa huyo anahitaji kwenda kutibiwa nchini India, ambapo kwa sasa anajipanga kifedha ili asafiri kwenda huko.

kajala-2
Akizungumza na gazeti hili, Kajala mwenyewe alisema kuwa anamshukuru Mungu, kwa hali aliyonayo sasa hivi kwani huko nyuma ilikuwa mbaya zaidi na kuna vitu vingi amevipunguza ili kuweza kunusuru maisha yake. 

“Ni kweli ni ugonjwa ambao nimeambiwa natakiwa kuwa nao makini laa sivyo maisha yangu yatakuwa hatarini, najaribu kufuata masharti lakini pia nina mpango wa kwenda kupata matibabu zaidi nchini India,” alisema Kajala.

 Kwa mujibu wa daktari mmoja aliyezungumza na gazeti hili, alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari na kama mhusika asipozingatia masharti, anaweza kufa kifo cha ghafla, huku akizitaja dalili zake kuwa ni mwili kuchoka na kuishiwa nguvu, kushindwa kupumua vizuri, hasa nyakati za usiku na kuvimba kwa baadhi ya viungo vya mwili, hasa miguu.

Comments are closed.