The House of Favourite Newspapers

Uingereza Yapata Waziri Mkuu Mpya Ambaye ni Mrithi wa Boris Johnson

0
Liz Truss

LIZ TRUSS ameshinda kinyang’anyiro na kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu Uingereza kupitia Chama cha Conservative.

Liz ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje alikuwa anachuana vikali na na Waziri wa zamani wa Fedha, Rishi Sunak.

Liz Truss, Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Truss ameshinda baada ya kupata kura 81,326 ikilinganishwa na mgombea mwenzake Sunak aliyepata kura 60,399.

Kesho anatarajiwa kumtembelea Malkia Elizabeth II huko Balmoral ili kupata idhini ya kuunda serikali yake.

Leave A Reply