The House of Favourite Newspapers

Kanye West Ausifia Wimbo wa Wizkid Esssence kama Wimbo Bora Kwenye Historia ya Muziki   

0
Kanye West Ameisifia ngoma ya Wizkid ya Essence kuwa ngoma bora ya muda wote

RAPPER kutoka Marekani Kanye West ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa hisia zake juu ya wimbo wa Wizkid “Essence” akiutaja kama wimbo bora toka historia ya muziki ianze hadi hii leo.

 

Wimbo huo ulitoka mwaka 2020, katika Album ya msanii huyo kutoka nchini Nigeria ya “Made in Lagos” ukaanza kupata mafanikio zaidi 2021 ukiuza zaidi ya nakala 2M nchini Marekani na pia umekuwa certified 2x Platnum na RIAA.

Kanye West na Wizkid

Siku ya Jumapili Rapper huyo kupitia ukurasa wake wa Instagramu aliandika hivi akionesha kuusifia sana wimbo huo:

“Best song in the history of music to date”

Kanye West

Katika post hiyo pia Kanye West aliusifia wimbo aliofanya akimshirikisha Beyonce ‘Church girl’ kama wimbo bora katika album yake, pia msanii huyo aliusifia wimbo wa Dj Khaled aliomshirikisha Rick Ross ‘God did’ kama wimbo bora wa mwaka.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa Mitandao.

Leave A Reply