The House of Favourite Newspapers

Ujumbe wa Haji Manara Kwa Wema Sepetu

0

 

Msemaji wa timu ya Simba, Haji Manara.

Manchester United imeendelea kutengeneza njia ya kuignia kwenye nafasi nne za juu baada ya kuifunga Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Ikicheza kwa kujiamini na kuonyesha soka zuri muda mwingi ilipata nafasi ya kufunga bao la kwanza kupitia kwa Marcus Rashford katika dakika ya saba baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Ander Herrera.

Licha ya kumuanzisha benchi straika wake tegemeo msimu huu Zlatan Ibrahimovic, Man United iliendelea kucheza soka zuri na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Herrera katika dakika ya 49.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho alionekana kuwa na mbinu nyingi za kuwabana wapinzani wake hasa Eden Hazard ambaye muda mwingi alikuwa akidhibitiwa na Herrera.


Kutokana na matokeo hayo Man United imeendelea kubaki nafasi ya tano kwa kufikisha pointi 60 wakati Chelsea nayo imebaki kileleni kwa kuwa na pointi 75.

Baada ya mechi hiyo msemaji wa timu ya Simba, Haji Manara alisema hivi kupitia akaunti yake ya Instagram Ufundi wa Hererra pale OT leo,,ni zaid ya kumuona Wema Sepetu akiwa na kanga moja iliyolowa maji @shaffih @edokumwembe @wemasepetu 😂😂😂 #GGMU 💪

Wema Sepetu (katikati).

SHOO YA HARMORAPA, JUMA NATURE, MSAGA SUMU, DULA MAKABILA DAR LIVE

Leave A Reply