The House of Favourite Newspapers

Ukimbizi, Uasi Hadi Mke wa Rais

0

SAFARI ya maisha ya mke wa Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye; Angeline Ndayubaha Ndayishimiye ni ndefu, baada ya kuzaliwa Juni 18, 1976 katika eneo la Kiganda, Wilaya ya Muramvya, nchini Burundi alikikuta ‘mikononi’ mwa ulimwengu ambao alianza kuutumikia.

 

Baada ya kupata elimu yake ya msingi na sekondari, Angelina alipoanza Chuo alijikuta akiishi ukimbizini kutokana na vuguvugu la uasi wa kikabila uliokuwa unaitafutana Burundi.

 

Mbali na maisha ukimbizi, mwanamke huyo alisema: “Haitoshi”, akajitumbukiza kwenye kundi la waasi la CNDD-FDD, lillilokuwa likipigana kuuondoa utawala wa rais wa wakati huo Pierre Buyoya, harakati ambazo zilitamatika mwaka 2003.

 

Akiwa kwenye mapambano huku akiishi ukimbizini, ndiko alikokutana na Jenerali Evariste Ndayishimiye ambaye naye alikuwa kwenye kundi la waasi, wakaanza kuyajenga mambo ya maisha yao.

 

Juni 18, 2020, Angelina alijipatia rasmi heshima ya kuwa mke wa rais baada ya mumewe kukabidhiwa madaraka kufuatia kifo cha mtangulizi wake Pierre Nkurunziza.

 

Katika ukurasa wake wa Twitter, Angelina ambaye ni mwanamke aliyejitoa kwa mengi kusaidia jamii kupita taasisi zake ya ‘Femme Intwari’ yaani Mwanamke Shujaa, aliandika:

“Nilikuwa mtafutaji wa amani nitaendelea kuwa mtafutaji wa maendeleo Burundi.”

Leave A Reply