The House of Favourite Newspapers

Mbowe Ataka Chanjo ya Corona Iwe Lazima kwa Watanzania Wote

0

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe leo Jumatatu, Julai 19, 2021 ameongea na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza kuhusu Polisi kuzuia kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana CHADEMA linalozungumzia hitaji la Katiba Mpya.

“Kama Polisi wakitaka wanikamate mimi Mbowe, tunalaani polisi kuvunja kongamano la BAVICHA juzi, Jumatano tuna kongamano la katiba walete vikosi kila sehemu, baada ya kongamano tutaanza mikutano ya hadhara nchi nzima hatutasubiri vibali….”

 

“Hatutaondoka hapa Mwanza, na wiki hii tufanya kongamano kubwa hapa. Sisi viongozi hatutaondoka Mwanza, na kama polisi wanataka kutukamata basi waanze kunikamata mimi Mbowe. Tutafanya makongamano haya nchi nzima hadi tupate katiba mpya….”

 

Mbali na hilo, Mbowe amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasaan aruhusu utoaji wa chanjo ya covid-19 uwe lazima kwa Watanzania wote na si hiari.

 

“Serikali inasema chanjo ya Covid-19 ni hiari ya mtu, akatayependa ndiye apewe, huu sio utaratibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchi za wenzetu chanjo ni lazima, tunamuomba Mama Samia aweke utaratibu wa chanjo kuwa lazima na inapaswa itolewe kwa kila mtu, huu ugonjwa unaua….

 

“Mgonjwa wa Covid-19 ukilazwa gharama ni zaidi ya Tsh. milioni 10 kwa wiki mbili, nimeuguza ndugu yangu Hospitali pale Moshi gharama ni kubwa, kwa siku anatumia mitungi minne kila mtungi ni elfu 30, ni Watanzania wangapi wanamudu? Gharama zinapaswa kubebwa na Serikali kwa kuwa WHO imetangaza kuwa huu ugonjwa ni janga la Taifa…” amesema Freeman Mbowe.

 

Aidha, Mbowe amemtaka Waziri wa Afya nchini humo Dk Dorothy Gwajima kujiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia vizuri mapambano dhidi ya corona. Mbowe ameyasema hayo leo na ambapo amedai Waziri huyo alikua anawadanga Watanzania kuhusu ugonjwa huo.

 

Mbowe amesema mpaka sasa hawajarudishiwa fedha zao kiasi cha Tsh. 350 licha ya kushinda kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi wa chama hicho na kwamba hawajui fedha hiyo wataipata lini na kwa utaratibu gani.

 

Leave A Reply