The House of Favourite Newspapers

Umaarufu Wa Kocha Senegal Haushikiki Urusi

Kocha pekee Mwafrika katika michuano ya Kombe la Dunia,  Aliou Cissé

 

ALIOU Cissé ndiye kocha pekee Mwafrika katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, umaarufu wake umekuwa mkubwa kutokana na kuiwezesha timu yake ya Senegal kushinda bao 1-0 dhidi ya Poland.

 

Ushindi huo ulikuwa ni pekee kwa timu za Afrika kabla ya michezo ya jana, hivyo kumpa sifa kocha huyo mzawa.

 

Cisse, alikuwa nahodha wa Senegal iliyotamba kwenye Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa kiungo mkabaji, anasubiriwa na wengi kuona kama ataendeleza makali yake keshokutwa Jumapili, watakapoivaa Japan kisha kumaliza hatua ya makundi dhidi ya Colombia.

Comments are closed.