The House of Favourite Newspapers

Umafia Mtupu Usajili Simba na Yanga

0

USAJILI unaofanywa na Simba na Yanga kipindi hiki cha dirisha dogoni umafia mtupu kwani hakuna ambaye
anataka kuona mchezaji wake
akiporwa.


Katika kuhakikisha kila
timu inafikia malengo yake, imefahamika kuwa, juzi Jumapili Yanga imemshusha kimyakimya kiungo mshambuliaji kutoka nchini DR Congo tayari kwa ajili ya kusaini mkataba wa kukipiga Jangwani.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo huyo ambaye kwa sasa jina lake wameamua kulificha kuogopa kuporwa na wapinzani, alitua Jumapili asubuhi na kupelekwa kwenye moja ya hoteli kubwa na ya kifahari iliyopo Posta, Dar es Salaam.


Mtoa taarifa huyo alisema kiungo
huyo jana Jumatatu alitarajiwa kukutana na mabosi wa Yanga mara baada ya timu kurejea Dar es Salaam ikitokea Sumbawanga kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.


“Jana (juzi) Jumapili asubuhi
alitua nchini kiungo mshambuliaji kutoka DR Congo aliyekuja kwa ajili ya kumalizana na uongozi wa timu yetu.


“Kama unavyofahamu Yacouba
(Songne) yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti, hivyo huyo jamaa ndiye atachukua nafasi yake na muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Frederick Mwakalebela alipoulizwa kuzungumzia hilo, alisema kwa sasa hana taarifa za ujio wa kiungo huyo.


Wakati Yanga wakifanya
hivyo, inatajwa kwamba Simba wamekomaa na mkata umeme, Samuel Sikaonga wa Zesco United ya Zambia.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

Leave A Reply