The House of Favourite Newspapers

Unilever yakamilisha kampeni ya Toa Mkono wa Ukaribu kwa kusaidia yatima, wazee

Meneja Bidhaa ya Omo ya Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (kushoto) akimkabidhi msaada wa sabuni, Sukari na Nguo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Children`s Home Msimbazi, Sista Etienne katika kuhitimisha Kampeni ya Kampuni hiyo ya Toa Mkono wa Ukarimu iliyofanyika Kipindi cha mwezi wa Ramadhani uliomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (katikati) akimkabidhi  msaada wa sabuni, sukari na nguo Ofisa Mfawidhi wa Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Jacklina Kanyamwenge katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki.  Wanaoshuhudia ni  Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Mmoja wa wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Vumilia Chambusho (kulia), akipokea msaada wa baadhi ya vyakula, nguo na sabuni kutoka kwa Meneja Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (watatu kushoto) vilivyotolewa na Unilever  katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo, Nunge,  Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni  Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Upendo Mkusa (kushoto) akisalimiana na baadhi ya wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge baada ya kukabidhi msaada wa sabuni, sukari na nguo vilivyotolewa na Unilever katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’.

Comments are closed.