The House of Favourite Newspapers

AFCON: Staa wa Misri Afukuzwa Kambini kwa Makosa ya Ngono

SHIRIKISHO la Soka la Misri (EFA) limetangaza kumtimua katika kikosi cha Timu ya Taifa ya nchi hiyo, kiungo Amr Warda, leo Jumatano kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

 

Warda (25), ambaye pia anakipiga katika Klabu ya PAOK ya Ugiriki, ametimuliwa katika Kambi ya Timu ya Misri ambao ni wenyeji wa Mashindano ya AFCON, baada ya kupatikana na makosa ya udharirishaji wa kingono kwa rundo la wanawake nchini humo.

Mchezji huyo ametimuliwa ikiwa ni siku moja baada ya kubainika kumdharirisha kingono mwanamitindo wa Misri aishiye Uingereza, Merhan Keller, ambaye ametoa ushahidi wa meseji za kingono, zisizo na maadili ambazo alitumiwa na Warda.

 

Baada ya Keller, wanawake wengine kibao (ambao ni wanamitindi) wamemiminika wakitoa ushuhuda wao wakisema Warda amekua akiwatumia meseji za kingono, kuwataka kimapenzi kwa lazima za kuwadharirisha.

Warda ametrendi kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram nchini Misri kutokana na sakata hilo ambalo limepelekea akina dada wengi ambao wameanika meseji za siri alizokua akiwalazimisha kutoka nao kimapenzi.

 

Inasemekana Warda amekuwa akiwatongoza akina dada hao na akikataliwa huwatukana matusi mabaya jambo ambalo wameamua kumtolea uvivu na kumwanika huku wakitaka EFA kumchukulia hatua mara moja kwa udharirishaji huo ili liwe funzo kwa wengine.

EFA imesema kuondolea kwa Warda kenye timu ya taifa ili kulinda nidhamu na heshima ya timu yao na nchi kwa ujumla huku kikosi kikibaki na wachezaji 22 ambao wataendelea na mashindano ya AFCON.

 

Warda amecheza mechi moja ya AFCON dhidi ya Zimbabwe ambapo Misri iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwny Uwanja wa Cairo. Pia alicheza kwenye mechi ya maanadlizi dhidi ya Taifa Stars ambapo Misri iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Kwa upande wake, Kocha wa Timu ya Taifa ya Misri, Ehab Lehita amethibitisha kutimulia kwa Warda lakini akalaumu kuwa sakata hilo limekuzwa sana na mitandao ya kijamii tofauiti kabisa na ukweli ulivyo.

Comments are closed.