The House of Favourite Newspapers

Upendo Music Festival kurindima kesho  

0

1.Kutoka kushoto ni msemaji wa tamasha hilo, Emmanuel Mabisa, Shaweji Somba na Isaack.

6.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

2.Mkutano ukiendelea.

3.

Viongozi hao wakitoa ufafanuzi wa jambo.

4.Waratibu wa tamasha hilo wakiwa katika picha ya pamoja.

5.Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili watakaotumbuiza siku hiyo, Levy Ngoy (kushoto) na Josiah  Sadock (katikati).

KESHO Jumapiliya Pasaka, Kampuni ya Legendary Music Entertainment itafanya  tamasha la pasaka litakalofanyika  katika Viwanja vya Leaders, Dar lengo la kuandaa tamasha hilo likiwa ni  kuwakusanya pamoja Wakristo wote ili waweze kumsifu Mungu na kufurahia kwa pamoja Sikukuu ya Pasaka pasipokujali dhehebu,  jinsia na umri .

Mratibu  wa shughuli  hiyo, Emmanuel Mabisa alisema kuwa tamasha hilo litaanza majira ya saa nne asubuhi mpaka saa tano kamili usiku. Hivyo kutakuwa na burudani kutoka kwa waimbaji na wasanii mbalimbali wa nyimbo za Injili pamoja na bonanza la michezo kwa mpira wa miguu na michezo mingineyo huku zawadi zitatolewa kwa washindi watakaopatikana pamoja na nyama choma, vinywaji na vyakula.

“Wasanii wa Nyimbo za Injili watakaoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Ambwene Mwasongwe, Faraja Ntaboba, Grolious Worship Team, Edson Mwasabwite, Sarah Shila, Emanuel Mbasha, Upendo Kihaile, The Joshua Generation, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, KKKT Kimara,  Angel Bernard, Calvary Band, Tumaini Shangilieni Choir kutoka Arusha, Chang’ombe Vijana Kwaya, The Next Level, Doxers Praise Team, Mise Recordians, Angel Magoti, Fridah Felix, The Voice  na wengineo.

“Kwa upande wa timu za mpira wa miguu zitakazopata nafasi ya kucheza ni timu 8 ambazo ni TBC Taifa, Kata ya 14 Jogging, Vikindu, KKKT Chang’ombe, Kariakoo, Times Radio, Biafra Jogging na timu ya Bills.

“Viingilio kwenye tamasha hilo vitakuwa 5,000 kwa Wakubwa na 2,000 kwa watoto na viti maalum 10,000.

“Mwisho kabisa tunapenda kuwakaribisha watu wote tushirikiane kwa pamoja katika tamasha hili la upendo ili tuweze kupata wasaa mzuri kufurahi hasa baada ya kumaliza kipindi cha mfungo wa siku 40 katika kukumbuka mateso ya Bwana Yesu kristo,”alisema.

 

  Na Denis Mtima/Gpl

 

Leave A Reply