The House of Favourite Newspapers

Usajili Kili Marathon Wapamba Moto

0
Washiriki wakiendelea kujisajili na wengine kuchukua namba zao za ushiriki.

Mashindano ya mbio za marathon yakiwa katika hatua za mwishoni kuanza kutimua vumbi Machi 1 mwaka huu Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, harakati za usajili nazo zimepamba moto ambapo leo wakazi wa jiji la Dar na mikoa jirani ambao waliofanya usajili kupitia mtandaoni Feburuari 22, 2020 walikuwa wakichukua namba zao za ushiriki zoezi lililofanyika Mlimani City, Dar.

 

Katika zoezi hilo wanahabari wetu walikuta raia wa nchi mbalimbali wakichukua namba zao baada ya kujisajili mtandaoni huku wengine wakiendelea kujisajili.

Usajili ukiendelea.

Akizungumza na wanahabari Wakala wa mbio hizo, Rajoon Datoo amesema mwaka huu mwitikio wa washiriki umezidi kuwa mkubwa kulinganisha na siku zilizopita na kusema mwaka huu wameboresha mambo mbalimbali ili kuendana na wakati.

Okemi Miriam raia wa Kenya akiwa na furaha wakati akiongea na waandishi wetu baada ya kupata namba ya ushiriki.

Baadhi ya washiriki waliozungumza na wanahabari wetu wakati wakichukua namba zao walisema mbio hizo ni sehemu ya kuimarisha afya zao na pia utalii wa ndani.

“Mimi hii ni mara yangu ya tatu kushiriki ambapo tangu niliposhiriki mara ya kwanza kwa jinsi nilivyoinjoi siwezi kuacha kushiriki tena yaani ni full burudani”. Alisema mmoja wa washiriki hao.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply