The House of Favourite Newspapers

USIKU MNENE WEMA, RUBANI WANASWA HOTELINI

MAPEMA mwaka huu kuliibuka taarifa za mwanaume mmoja ambaye ni rubani wa ndege aitwaye Hamdan Za­kwani ‘Danzak’ aliyetangaza kumuoa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye wikiendi iliyopita walinaswa ‘live’ hotelini.

MECHI YA STAR VS UGAN­DA

Kabla ya kunaswa wakizama hotelini usiku mnene wa Jumapili iliyopita, Amani liliwapiga chabo Wema na Danzak wakijiachia kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda The Cranes ijapokuwa hawakujiachia waziwazi ili watu wasiwaone ila kuna wakati walishuhudi­wa wakibadilishana namba za simu. Wawili hao walishuhudiwa wakipagawa na ushindi wa Taifa Stars wa bao 3-0 dhidi ya Uganda katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Baada ya hapo sasa, Amani liliamua kuwafuatilia hatua kwa hatua kujua kina­choendelea kati ya wawili hao kwani umepita muda mrefu bila kujua walifikia wapi kwenye masuala yao ya uchumba.

NDANI YA SERENA

Hata hivyo, nyapianyapia ya gazeti hili ilizaa matokeo baada ya kuwaona wawili hao wakiingia hotelini wak­iwa pamoja pale Serena Hotel maeneo ya Posta jijini Dar, huku wakiwa na shang­we kama lote kutokana na ushindi wa Stars. Wakiwa ndani ya Ser­ena Hotel, wawili hao hawakupata chansi ya kujiachia ‘praiveti’ kwani kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakishangilia ushindi wa Stars.

HAOO SEA CLIFF

Baada ya kuona gozigozi, Wema na Danzak walion­doka hotelini hapo ambapo walielekea maeneo ya Hoteli ya Maison Sea Cliff iliyopo Masaki, jijini Dar ki­sha walijiachia watakavyo.

Pamoja na usiku kuzidi kuwa mnene, lakini shang­we la wawili hao haliku­komea hapo kwani safari iliendelea ambapo walik­wenda kuhitimisha kwenye hoteli moja iliyopo maeneo ya Msasani jijini Dar. Likiwa hotelini hapo, Am­ani liliwafotoa picha kisha liliwasikilizia wawili hao watoke, lakini hawakutoka hadi linaanua jamvi eneo hilo.

WEMA ATAFUTWA HEWANI

Kesho yake, yaani Ju­matatu wiki hii, Amani lilimtafuta Wema ili kujua ameamkaje kutokana na uchovu wa kushangilia ush­indi wa Stars na kilichoen­delea kati yake na Danzak, lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Alipotafutwa Danzak na kusimuliwa taarifa zake na Wema hatua kwa hatua tangu Uwanja wa Taifa, Serena, Sea Cliff hadi hotel­ini hapo, alicheka kisha akajibu kwa kifupi: “Mambo mazuri hayahitaji haraka.”

TUTOKAKO…

Mapema Januari, mwaka huu, baada ya jamaa huyo kuonesha nia ya kumuoa Wema, mama wa mrembo huyo, Mariam Sepetu alim­karibisha kufika nyumbani kwa ajili ya taratibu ny­ingine. Hata hivyo, hapo katikati ulipita ukimya mrefu hivyo haikujulikana kama Danzak alikwenda kutimiza taratibu za mama Wema kwa ajili ya kumuoa mlimbwende huyo wa Taji la Miss Tanzania mwaka 2006/07.

DANZAK NI NANI?

Ni Mtanzania ambaye kabla ya kwenda masomoni nje ya nchi ame­wahi kufanya kazi za muziki ka­tika Kundi la TNG Squard lililokuwa likiundwa na wasanii Agustino John ‘Latino Man’ na Malicki Bandawe kutoka jijini Tanga. Inaelezwa kuwa, mbali na kurusha ndege, bado shu­ghuli za kimuziki ziko kwenye damu ya Danzak na kwamba hata alipomaliza masomo ya uru­bani, alitua Bongo na kutunga na kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Fall In na Kichaa.

Comments are closed.