The House of Favourite Newspapers

Usiku wa Ya Kale ni Dhahabu… Dar Live kuweka historia Muziki wa Taarab

0

khadija_kopa1

Stori: Mwandishi Wetu

MEI 21, mwaka huu, Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar utaweka historia kwa mara ya kwanza kunako Muziki wa Taarab pale zitakapopanda bendi zaidi ya ishirini na kupiga bonge moja la shoo.

Akizungumza na Uwazi Showbiz, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliwataja wakali watakaoweka historia kuwa ni Leila Rashid, Hadija Yusuf, Bi Mwanahawa, Joha Kassim kutoka Jahazi Modern, Hadija Kopa, Otham Sudi, Mwanaidi Shaban kutoka Muungano, Shakira kutoka J.K.T, Misambano na Kisauji kutoka Babloom.

“Utakuwa ni usiku wa kukumbukwa na kila mmoja kwa maana kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikundi hivyo kukutana katika jukwaa la Dar Live,” alisema Mbizo.

Wakali wengine wanaotarajiwa kuwepo ni Sabaha Mchacho, Sihaba Juma, Hassan Soud, Thabit Abdul, Bi Afua, Sizya Mazongela, Mustafa, Sihaba Juma, Zubeda Mlamali na wengine kibao.

Shoo hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Airtel, kupitia huduma yao ya kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap inayopatikana jijini Dar kwa sasa.

Leave A Reply