The House of Favourite Newspapers

Utafiti wa WHO Wathibitisha Watu Wanaoketi Muda Mrefu Wanakufa Mapema

0

TAFITI mbalimbali zilizofanywa na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinathibitisha kwamba, watu wanaoketi kwa muda wa hadi saa nane kwa siku wapo kwenye hatari ya kufa mapema.

Kwa mujibu wa ripoti hizo za madaktari na wataalam, kuketi kwa muda mrefu huathiri mwendo wa mzunguko wa damu mwilini.
Wanasema mtindo wa maisha wa kuketi muda mrefu, unachangia asilimia 30 ya maradhi ya moyo na kati ya asilimia 20-25 ya saratani ya matiti, kibofu na mapafu.

Daktari Mounir Dia wa Senegal anasema; “Kuna viungo vingi vya mwili ambavyo huathiriwa kwa kuketi muda mrefu.
“Mtu asipoyafanya mazoezi, kuna uwezekano mkubwa wa mapigo ya moyo kuongezeka na ni rahisi kupata magonjwa ya moyo na kusababisha kifo.”

Wataalam wanasema kuwa kama umezoea kushinda kwenye kiti kazini kwa kipindi kirefu, yafuatayo ni mambo ambayo unaweza ukayafanya ili kujinusuru;

Kwanza unaposhuka kwenye basi, daladala au treni, hakikisha unashuka mbali na ofisini ili upate nafasi ya kutembea na kama unaendesha gari, hakikisha unaliegesha mbali kiasi na mahali pa kazi ili utembee.

Pia wanashauri kwamba badala ya kutumia lifti, hakikisha unatumia ngazi kisha simama kwa dakika moja, kila baada ya saa moja au dakika tano hadi 10 kwa kila dakika 90.

WHO inapendekeza mazoezi ya dakika 30 kwa watu wazima na saa moja kwa watoto, bila hivyo, inachukuliwa hufanyi mazoezi.

Stori: Sifael Paul

Leave A Reply