The House of Favourite Newspapers

Utambulisho Wa Ngoma Simba Sapraiz Kubwa

0
Fabrice Ngoma

IMEBAINIKA kuwa uongozi wa Klabu ya Simba umepanga kumtambulisha kiungo wao mpya, Fabrice Ngoma kama mchezaji wa mwisho kutokana na kuamini kuwa ndio usajili ambao utatikisa zaidi msimu huu.

Ngoma anaripotiwa kuvunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan kutokana na ligi kusimama kufuatia machafuko lakini hata hivyo klabu hiyo imekuja juu ikidai hajafuata kanuni zinazotakiwa, hivyo Simba wameenda kumalizana kistaarabu ili imbibe mwamba huyu.

Chanzo cha ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumatatu kuwa: “Simba wamekamilisha tayari taratibu za sajili zao nyingi hivyo kilichobaki kwa sasa ni utambulisho wa wachezaji ambao bado hawajatambulishwa.

“Ukiangalia mipango ya uongozi ni kuhakikisha kuwa wanamtambulisha Fabrice Ngoma mwishoni na ndio maana utaona tayari kuna wachezaji wametambulishwa mapema lakini Ngoma bado hajatambulishwa.

“Hiyo ni mipango ambayo wanaona kuwa Ngoma akitambulishwa mwishoni litakuwa jambo kubwa kwa kuwa ni usajili ambao uliimbwa sana na kutokana na kuhusiswa na Simba kuwapokonya Yanga mchezaji huyo,” kilisema chanzo hiko

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally yeye ameliambia Championi Jumatatu kuwa: “Simba msimu huu kila usajili ni usajili mkubwa na hakuna sijui usajili huu wa kawaida wala ule mkubwa kuliko huu, kila usajili utakuwa tishio jambo ambalo wanasimba wanatakiwa kulifanya ni kuendelea kuwa karibu na sisi kwani tutashusha vyuma vya maana.”

Na Marco Mzumbe

WANNE WAFUNGA USAJILI YANGA/ BAADA ya MALONE, VYUMA 3 VIMEBAKI SIMBA, MIQUISSONE ATAJWA…

Leave A Reply