The House of Favourite Newspapers

Utani Dhidi ya Trump Kumuingiza Johnny Depp Matatani

0

NI UTANI WA NGUMI! Muigizaji mwenye jina kubwa Hollywood, Johnny Depp anaweza kuingia matatani baada ya kutoa utani jukwaani wa kumuua Rais wa Marekani, Donald Trump ili awe msanii wa pili kufanya hivyo nchini humo.

Staa huyo anayetamba na Muvi ya Pirates of Carribeans V iliyoingia sokoni mwezi huu aliingizia utani huo alipokuwa katika Tamasha la Glastonbury nchini Marekani kiasi kwamba alishangiliwa na umati wa watu uliokuwa mahali hapo.

“Nadhani anahitaji kusaidiwa!” alisema na kuongezea:

“Hivi mara ya mwisho ni lini kwa muigizaji kumuua rais wa Marekani?” aliuliza swali lililopokelewa kwa shangwe zaidi na watu waliokuwa mahali hapo.

Ikumbukwe tu kwamba mara ya mwisho kwa rais wa Marekani kuuliwa na muigizaji ilikuwa ni mwaka 1865 ambapo aliyekuwa rais, Abraham Lincoln aliuawa na jamaa anayeitwa John Wilkes Booth huku rais wa Marekani wa mwisho kuuawa na mtu wa kawaida alikuwa John F. Kennedy mwaka 1963.

Kwa utani huo, inawezekana Depp akaingia matatani kwa utani wake huo ambao ulionekana kuwafurahisha watu wengi waliokuwepo mahali hapo.

Na: Nyemo Chilongani

Leave A Reply