The House of Favourite Newspapers

Utata Idadi Ya Vifo Ukraine

0

 

WAKATI mapigano kati ya Urusi na Ukraine yakiingia siku ya tatu leo, majeshi ya Urusi yakiwa yameuzingira Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv bado kuna utata mkubwa kuhusu idadi kamili ya vifo ambavyo vimetokea mpaka sasa.

 

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Liashko inaeleza kwamba mpaka leo Jumamosi, watu 198 raia wa Ukraine wamefariki dunia kutokana na uvamizi wa Urusi, wakiwemo watoto watatu.

 

Waziri huyo ameongeza kuwa watu wengine 1,115 wamejeruhiwa wakiwemo watoto 33 na kuongeza kuwa maelfu ya wananchi wa Ukraine hususan wanawake na watoto, wanaendelea kuvuka mpaka kuingia nchini Poland kuomba hifadhi.

 

Hata hivyo, taarifa hizo za waziri huyo wa afya, hazijafafanua kwamba watu 198 waliouawa ni raia pekee au ni mchanganyiko wa raia na wanajeshi.

 

Wakati waziri huyo akieleza hivyo, vyanzo vingine katika jeshi la Ukraine ambavyo havijathibitishwa, vimeeleza kuwa wanajeshi takribani 3,500 wa Urusi wameuawa katika vita hiyo, taarifa ambazo zimepingwa vikali na maafisa wa Urusi.

Leave A Reply