The House of Favourite Newspapers

Mrembo: Nataka kuzaa na Harmonize

0

MREMBO mmoja ameibuka nchini Tanzania akitokea Dubai; lengo lake likiwa ni kumtafuta msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul au Harmonize.

Mrembo huyo ambaye jina lake kamili halijapatikana bado, anasema amekuwa akivutiwa mno na mwonekano wa Harmonize ambao umekuwa ni kama sumaku inayomvuta kwake akitamani awe mpenzi wake na amzalie mtoto.

 

Anasema kuwa, amekuwa na ndoto ya kuzaa na Harmonize au Harmo; ndoto ambayo imemlazimu kuachana na mpenzi wake na kutua Tanzania kumtafuta jamaa huyo angalau amweleze shida yake.

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii mrembo huyo anakiri kutamani kuwa na Harmonize na kueleza kuwa yeye hatafuti kiki ila anachotaka ni kupata ujauzito wa msanii huyo.

Anaeleza kuwa, ameshawaeleza wazazi wake sababu za kufika Tanzania na wote wamekubaliana naye. “Nataka kuzaa na Harmonize, nataka niwe na damu yake kutokana na ninavyomkubali na kumpenda.

Hicho ndicho kimenitoa Dubai kuja hapa (Tanzania), sitaki kiki, sitaki pesa, pesa ninazo, najua kutafuta pia. Kwa hiyo ninachotaka nikutane naye,” anasema mrembo huyo.

Anaendelea kufunguka; “Mimi nina mpenzi wangu, kwa sasa yuko Dubai, kulingana na jinsi nilivyomzoea Harmonize wakati mwingine namtaja, kuna kipindi nikiwa na mpenzi wangu badala ya kumtaja yeye nikamtaja tu Harmonize.”

 

Kauli ya mrembo huyo imejiri wakati huu Harmonize akiwa anapewa mapenzi motomoto na mpenzi wake wa sasa, Briana; raia wa Australia.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply