The House of Favourite Newspapers

Uwoya Ahofia Mzuka wa Masogange!

Irene Uwoya

MREMBO aliyekuwa shosti mkubwa wa marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’, Irene Uwoya, amesema baada ya rafiki yake huyo kufariki, amekuwa akipata shida sana kukaa peke yake kwa hofu ya kutokewa na rafiki yake huyo.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Uwoya alisema, kwa jinsi walivyokuwa karibu na Masogange, amekuwa akiwaza mengi na ndiyo maana ameshindwa kabisa kuishi katika nyumba ile waliyokuwa wanaishi jirani na mrembo huyo, maeneo ya Makongo Juu jijini Dar.

“Nahofia kweli jamani kutokewa na Masogange. Kwa sasa imenibidi niwe mtu wa kujichanganya sana ili nisiwe namkumbuka Masogange,” alisema Uwoya.

Comments are closed.