The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi: Shigongo Achangisha Mamilioni Harambee Kanisa la Aic Chang’ombe

  shigongo-3

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa semina fupi iliyoambatana na historia ya maisha yake.

shigongo-1

Shigongo akizidi kutoa semina kwa waumini wa Kanisa la African Inland.

shigongo-2

Waumini wa Kanisa la African Inland wakimsikiliza Shigongo.

shigongo-4

Shigongo akihamasisha kuchangia ujenzi wa kanisa.

JANA Jumapili, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo amechangisha mamilioni katika harambee iliyofanywa na Kanisa la African Inland.

Ujenzi kamili wa kanisa hilo ulianza rasmi Oktoba 14, mwaka 2014, ambapo umechukuwa miaka miwili ukiwa umegharimu hadi sasa kiasi cha zaidi ya milioni 570 za Kitanzania.

Awali, kulikuwa na uzinduzi wa ujenzi wa kanisa hilo na mara baada ya hapo, Shigongo ambaye alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, alipewa nafasi ya kutoa neno mbele ya wageni waalikwa, wachungaji kutoka sehemu mbalimbali na waumini wa kanisa hilo ambapo aliwekeza kwa Mungu kiasi cha milioni kumi akiwa naimani na kuwasihi waumini wote walikuwemo wategemee baraka za Mungu kwa kile walicho mtolea.

Akizungumza katika uzinduzi na harambee hiyo, Shigongo alitoa semina fupi iliyoambatana na historia ya maisha yake ambayo iliwagusa waumini wengi na kupelekea kupata mchango wa mamilioni ya pesa.

Shigongo pia alifundisha kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba kwa Mungu na kumtolea kwa kujitoa kwa ajili yake.

“Katika siri kumi za mafanikio niligundua kuna umuhimu wa kumtolea na kujitoa kwa Mungu na hiyo ikawa ni moja kati ya sheria zangu za mafanikio.

Stori / Picha: Kelvin Shayo na Hilaly Daud / Global TV Online

Comments are closed.