The House of Favourite Newspapers

TECNO YAZINDUA DUKA JIPYA LA ‘EXPERIENCE CENTER’ SAMORA DAR (Picha + Video)

Naibu waziri Mawasiliano na Uchukuzi Mheshimiwa Atashasta Nditiye,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.

KAMPUNI ya simu za mkononi, TECNO inayofanya kazi chini ya TRANSSION HOLDINGs imezidi kutanua wigo  wa soko la simu nchini kwa kufungua duka jipya maarufu la “Experience Center’’ jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Samora,  Jumamosi jana Machi 24.  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,  Atashasta Nditiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye,  akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Waziri huyo alishiriki zoezi la kukata utepe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TECNO, Daniel Xu na Mkurugenzi  wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Mkurugenzi Mkuu wa TECNO, Daniel Xu (katikati) akizungumza jambo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa TECNO nchini, Daniel Xu alisema “Ni furaha kujumuika nanyi katika uzinduzi wa duka jipya la  TECNO “Experience Center”, ambapo wateja watapata fursa ya kununua bidhaa, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi, sifa na mifumo mbalimbali ya simu, lakini pia huduma ya matengenezo (after sales service) kupatikana papohapo dukani.

 

Aidha Xu, aliongeza kwamba uzinduzi huo unatoa fursa nyingine ya ajira kwa vijana wa Tanzania ili kuwainua kiuchumi, ambapo zaidi ya vijana 500 wameshaajiriwa kwenye kampuni ya TECNO.

Naibu Waziri Nditiye akiendesha zoezi la bahati nasibu, na baadaye alikabidhi zawadi kwa wateja waliojishindia zawadi kabambe kupitia droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa baada ya uzinduzi huo.

Kwa upande wake,  Nditiye  alizunguka  sehemu mbalimbali za duka hilo kujionea huduma mbalimbali zinazopatikana ambapo alisema kuwa TECNO imekuwa chachu ya kukuza teknolojia na mawasiliano ambapo alisema aslimia 94 ya wananchi wana mawasiliano nchini, lakini akapongeza Kampuni ya TECNO kwa kitendo chake cha kuwapa  watumiaji  elimu ya namna ya kutumia simu kuepuka uhalifu.

Nditiye (wa tatu kulia) akiwa katika picha na  baadhi ya washindi wa bahati nasibu..

Kampuni ya TECNO inawakaribisha wateja wote katika duka lao jipya linalopatikana Samora, Posta,  jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.