The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa Gazeti la Spoti Xtra Waitikisa Arusha, Sasa Mtaani Jumapili Hii

Chokala akifungukia Spoti Xtra.

KAMPUNI ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Amani, Ijumaa, Uwazi, Risasi na Championi imezindua Gazeti  Jipya na Bora la Michezo na Burudani ‘Spoti Xtra’, uzinduzi ukifanyika katika mikoa wa Arusha na Dar es Salaam leo Ijumaa, Desemba 15, 2017.

Wakazi wa mkoa wa Arusha wamepokea uzinduzi wa Spoti Xtra kwa ari kubwa huku wengi wao wakilisubiri kwa hamu siku ya Jumapili ili kushuhudia ubora wake na namna litakavyokuwa tofauti na magazeti mengine ya michezo hapa nchini.

 

Uzinduzi ulivyofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ujio wa Spoti Xtra wakati akifanya mahojiano ya moja kwa moja na Kituo cha Redio maarufu na chenye wasikilizaji wengi zaidi mkoani Arusha na mikoa mingine cha Triple A FM, Mwakilishi wa Kampuni ya Global Publishers, Choks Chokala amesema;

“Ili tufunge mwaka vizuri, Kampuni ya Global Publishers tumeamua tuje na Gazeti la Spoti Xtra, hili ni gazeti la Michezo litakalokuwa linatoka Jumapili, hapo mwanzoni hatukuwa na Gazeti siku ya Jumapili. Hivyo wasomaji wetu waelewe kuanzia leo kwamba kila Jumapili tutakuwa na Gazeti hili la Spoti Xtra ambalo limekuja kumaliza kiu yao na hamu ya kufahamu mambo mbali mbali yanayohusu michezo.

Wahariri wa michezo wa Global Publishers na wafanyakazi wenzao wakijiselfisha baada ya uzinduzi huo.

“Spoti Xtra limekuja kuziba hilo pengo la Jumapili ambapo hakuna gazeti, hili litakuwa dude zaidi, bei yake ni Sh. 500 tu. Tumejipanga vizuri sana, wanendelee kusoma,” alisema Chokala.

Gazeti hili litakuwa na waandishi waliobobea, wachambuzi mahiri na watalichambua soka na michezo yote kwa makini. Takwimu zote za soka kuanzia Ulaya, Afrika na Tanzania zitakuwepo tena kwa ubunifu wa hali ya juu.

Gazeti la Spoti Xtra litakuwa mtaani kila Jumapili, na litaanza rasmi kutoka kuanzia keshokutwa Jumapili, Desemba 17, 2017. Kaa mkao wa kula! Spoti Xtra, Hapa ni Uhondo Tu!

 

Gazeti Jipya la Michezo, ‘Spoti Xtra’ Lazinduliwa Dar, Mtaani Kila Jumapili- (Video)

Comments are closed.