The House of Favourite Newspapers

 UZINDUZI WA ‘MAMA WA HIYARI’ ULIKUWA MOTOOO!

Sabaha Salum Muchacho akiwanogesha mashabiki wa kibao chake maarufu kiitwacho Sitaki.

Kundi la First Class Modern Taarab la jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo limezindua albamu yake ya kwanza iitwayo Mama wa hiyari.

Uzinduzi huo uliofanyika Travertine Hotel iliyopo Magomeni jijini Dar ulihudhuriwa na umati wa mashabiki wakiwemo wakongwe wa muziki huo akiwemo Sabaha Salum Muchacho, Bi. Mwanahawa Ally, Mwanamtama Amiri na wengine wengi.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbiramoto.

Matukio katika Picha: 

Mpiga gitaa la kuongoza (solo) wa bendi hiyo, Emeraa Solo na Fatma Masanja anayeimba wakiwanogesha mashabiki.
Muimbaji mkongwe, Mwanahawa Ally (kushoto)  akifuatilia burudani ya uzinduzi huo.
Aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbiramoto (kulia) akilitakia mafanikio mema kundi hilo jipya na kuwaambia wanamuziki wake wakaze buti ili kutimiza malengo yao.
Shabiki akimtunza mmoja wa waimbaji wa kundi hilo baada ya kumkuna na kibao alichokuwa akiimba.

Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL    

Comments are closed.