The House of Favourite Newspapers

V- Money: album ni muhimu sana kwa msanii

0

vanessaStori: Boniphace Ngumije

MWANADADA anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa burudani Bongo, Vannesa Mdee ‘V Money’ amesema kuwa moja ya vitu muhimu kwa msanii ni kuhakikisha anatoa album na kuisimamia ifanye vizuri sokoni ili kujitengenezea heshima, uaminifu, lakini zaidi kutengeneza nafasi ya kupata madili makubwa ambayo sana huzingatia mauzo ya album ya msanii.

Akichonga na mtandao huu, V-Money aliongeza kuwa kwa upande wake kwa sasa yuko ‘bussy’ kuandaa albam yake inayokwenda kwa jina la Money Mondays ambayo ndani yake itakuwa na ‘surprise’ kibao ambazo hayuko tayari kuziweka wazi kwa sasa.

“Wasanii wamekuwa na kasumba ya kuogopa kufanya album kwa mtazamo kuwa haziuzi, lakini mimi ninachoamini si kweli kuwa album haziuzi, ila wasanii wengi wamekosa mbinu za kuuza album. Kwa upande wangu ninawashauri watoe album kwa sababu ni muhimu kwao kibiashara,” alisema V- Money.

Leave A Reply