The House of Favourite Newspapers

VEE MONEY ATOBOA SIRI YA KUANDAA SHOO ZAKE

 

Vanessa Mdee ‘Vee Money

MWANAMUZIKI wa kimataifa, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, amesema siri ya kuandaa shoo zake mbali na kufikisha kazi zake kwa mashabiki wengi zaidi ni kuwaonyesha wanamuziki wengine ambao ni wasanii wakubwa kwamba inawezekana kujitegemea na kufanya kile unachohitaji kwenye muziki.

Vee Money, ambaye wikiendi hii alikuwa na shoo kwenye Ukumbi wa Next Door Arena, ikiwa ni mwendelezo wa ‘tour’ yake ambayo aliipa jina la In Love With Money, ambapo amezunguka kwenye mikoa mbalimbali Bongo, aliiambia Risasi Vibes kwamba kikubwa ni wasanii kujituma na kufahamu nini wanatakiwa kufanya kwenye muziki.

“Watu wanaweza kujiuliza kwa nini nimeandaa tour yangu hii. Siri ni kwamba nilihitaji kuwafikia mashabiki wangu, kazi zangu kufika kwao lakini pia kuwaonyesha wasanii kwamba inawezekana. Msanii kujisimamia na kufanya hiki nilichokifanya mimi,” alisema Vee Money.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.